Web Templates
Country Profile  
Attractions  
Home  
 
 
 

  Sign Up
News and Events Visa Guestbook Trade Tourism Investment
 
Tanzania
  ABOUT MISSION
  ABOUT TANZANIA
  TANZANIA ATTRACTIONS
  BUSINESS
  EMBASSIES 
  VISA
  NEWS & EVENTS
  GALLERY
  GUEST BOOK
  REGISTRATION
  VISA FORM
  PASSPORT



PASIPOTI ZA TANZANIA

Kufuatia maulizo mengi kuhusu utoaji wa Pasipoti Mpya, ufuatao ni utaratibu wa kushughulikia zoezi hili kwa Watanzania waishio Uingereza na Ireland.

Pasi zote zilizotolewa awali zenye kurasa 36 zimesitishwa kutumika tena kwa safari; kuanzia tarehe 30 September 2005. Kwa mantiki hiyo basi, pasi hizo sio Pasi halali za safari.

Kwa Mtanzania yeyote mwenye makazi yake hapa Uingereza ama Ireland; iwapo atapata safari ya dharura, kabla ya kupatiwa Pasi mpya ya kusafiria ama kubadili Pasi ya Kusafiria ya zamani, anatakiwa awasiliane na Afisa Uhamiaji, Ubalozini London; ili kuandaa taratibu za kupatiwa Pasi ya Dharura ya Kusafiria.

A. UPATIKANAJI WA FOMU ZA PASI MPYA

Mwombaji anaweza kuja Ubalozini ili kununua fomu au atume GB Sterling Pounds (£) 5.00,- (malipo ya fomu kwa rejista). Aidha, alete bahasha yenye anuani yake iliyobandikwa stampu za rejista ili apelekewe fomu. (Aweke pound 5.00 malipo ya fomu)

  • Wale watakaopenda kuja Ubalozini kununua fomu na kurudisha fomu wazingatie utaratibu ulioelezwa hapa chini kifungu B.
  • Kila fomu ina namba maalum (Unique Identity No.), haiwezi kutumika kwa watu wawili. Mwombaji asithubutu kutoa nakala (photocopy) ili itumike kwa mwombaji mwingine.
  • Watanzania wanaokwenda nyumbani siku za karibuni wanashauriwa na wanaruhusiwa kuomba pasipoti mpya wakati wakiwa nyumbani katika ofisi za uhamiaji Tanzania. Kufanya hivyo kutawaharakishia kupata pasipoti hizo na kupunguza gharama za kufuatilia ubalozini London.
  • Inatahadharishwa kuwa fomu za uombaji pasipoti zilizokosewa au kufutwafutwa hazitakubalika itabidi mwombaji anunue fomu nyingine. Ni vema kabla ya kujaza fomu mwombaji atoe nakala (photocopy) ya fomu aijaze kwanza kila kipengele ili baadaye anakili katika fomu aliyopelekewa kuepuka makosa ya kufutwafutwa na kununua fomu nyingine.

B. UTARATIBU WA KUOMBA PASI

Malipo yakipokelewa, mwombaji atapewa fomu au atapelekewa fomu husika ambayo ataijaza BILA kuweka sahihi yake katika sehemu ya sahihi, ukurasa wa kwanza na wa pili.

  • Jaza ukurasa wa kwanza na wapili tu, yaani kifungu cha 1 - 5 tu. Pia jaza karatasi ya alama za vidole. Tunasisitiza kuwa uje na fomu zimejazwa tayari. Sehemu ya anwani ni yoyote unayoitaka wewe.
  • Sehemu yenye habari za wazazi wa mwombaji zijazwe kikamilifu. Sehemu za mahali pa kuzaliwa zijazwe kama fomu inavyoeleza. Kama hufahamu vizuri uliza wenzako kabla ya kuja. Kujaza sehemu ya mama mzazi, jaza majina yake ya ukoo na sio majina yake ya kuolewa. 

 

Mwombaji anatakiwa kuleta:

  1. Fomu yake, na iliyokwishajazwa tayari. Kama huelewi uliza wenzako.
  2. picha tano (5) za pasipoti zenye `background' ya rangi ya ` blue' au rangi ya maji ya bahari. Picha hizo lazima ziwe za hivi karibuni na zenye kuonyesha masikio yote mawili.
  3. Nakala au kivuli cha Pasi ya zamani (photocopy) kurasa tatu (3) za kwanza,ukurasa wenye kibali cha makaazi (visa) na ukurasa wa mwisho wenye DN au IF.
  4. Muda wako wa kuchukuliwa alama za vidole ni kati ya saa 4 hadi saa 6.30 alasiri. Baada ya hapo hakuna huduma hiyo.


Wakati wa kujaza fomu `Section 2' tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa wazazi ni LAZIMA.

*FOMU IJAZWE KWA HERUFI KUBWA!

  • Kama kuna sababu ya kubadilisha jina lazima hati husika za sababu ya kubadili jina ziletwe - k.m. cheti cha ndoa, au hati maalum za kubadili majina (deed poll).
  • Kama pasipoti imepotea LAZIMA ripoti ya polisi na `affidavit' (hati ya kiapo) mbele ya mwanasheria zitumwe pamoja na fomu na maelezo yako bunafsi ya ulikozaliwa, kuishi, ilikotolewa pasi na lini, na imepoteaje.
  • Acha au usijaze kipengele cha sita (6) katika fomu kwa kuzingatia Maelezo Muhimu kwenye kipengele cha pili (2) - waliotajwa hawapatikani nje ya Tanzania.

C. ALAMA ZA VIDOLE

Katika utoaji wa pasipoti mpya lazima mwombaji achukuliwe alama za vidole (`finger prints') na kuweka sahihi kwa mkono wake mwenyewe mbele ya afisa mhusika.

Kufanyiwa alama za vidole, Mwombaji anatakiwa kuomba kupewa siku ya ahadi (Appointment).Hivyo Mwombaji anatakiwa kuwasiliana na Ubalozi kwa kupiga simu, ama kutuma barua pepesi. Fomu zinaweza kuchukuliwa siku yoyote, na Mwombaji haitaji ahadi (Appointment) ili kupata fomu.

    • Mwombaji anatakiwa aje UBALOZINI ili kutia sahihi fomu na kuchukuliwa alama za vidole.

      Mwombaji atatakiwa alipe jumla ya GB Sterlin Pounds (£ ) 45 [5 kwa ajili ya fomu na 40 kwa ajili ya pasipoti].- malipo ya pasipoti mpya.
    • Maombi yatashughulikiwa na kupelekwa haraka Makao Makuu ya Uhamiaji Dar es Salaam.
    • Pasi mpya zitatolewa Makao Makuu ya Uhamiaji, Dar es Salaam na kuletwa Ubalozini.
    • Pasipoti ya zamani itabidi ifutwe hivyo mawasiliano na Ubalozi ni muhimu.
    • Utaratibu mzima wa kushughulikia unatazamiwa kuchukua wiki sita (6) au zaidi.
    • gharama GB Sterlin Pounds (£ ) 45,- yaani £ 5 za fomu na £ 40,- pasipoti.

    TAHADHARI:

Pasipoti mpya zitatolewa kubadilisha zile ambazo zilizotolewa kihalali na zenye kumbukumbu za utoaji kwa raia wa Tanzania. Siyo kwa wale wenye uraia wa nchi nyingine walio na pasipoti mbili. Kisheria nchi yetu hairuhusu `dual citizenship'; kufanya hivyo ni kinyume cha sheria. Akigundulika mwombaji mwenye uraia wa Tanzania na nchi nyingine atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Aidha pasi za Tanzania hazitolewi kwa watu wenye sifa za ukimbizi. Kama kwa udanganyifu au bahati mbaya watajwa hapo juu walipata pasi zetu wanamiliki kinyume cha sheria na tutatangaza kuzifuta.

  • Watoto watapewa pasipoti zao kwa kuzingatia utaratibu ulioelezwa.
  • Watoto wa umri usiozidi miaka mitano hawatachukuliwa alama za vidole vyote.

 

D. WALIOPOTEZA PASI

Kwa waliopoteza Pasi, LAZIMA kuwasilisha pamoja na maombi yako vitu vifuatavyo:

  • Ripoti ya polisi kuthibitisha kupotea/kuibiwa kwa Pasi ya Mwombaji
  • Mwombaje atoe maelezo binafsi kwa maandishi wakieleza yafuatayo:
    1. Taarifa za Pasi iliyopotea,
    2. Mazingira ya Pasi ilivyopotea/kuibiwa,
    3. Mahali Pasi ilikotolewa
    4. Tarehe na mwaka Pasi ilipotolewa, Namba ya Pasi na DN.
    5. Tangazo la gazeti kuhusu kupotea pasi.          
  • Ni juu ya mwombaji kutafuta taarifa hizo, asije kuuliza ubalozini atakavyopata vitu hivyo.
  • Kwa mtu asiye na uthibitishi wowote ni vigumu kweu kumpa huduma. ukishindwa kabisa wasiliana na wazazi nao wapeleke uthibitisho huo uhamiaji makao makuu.

Taratibu za kawaida za kuomba Pasi zitafuata baada ya Mwombaji kukamilisha maelekezo ya hapo juu.

E. KUJUMUISHA WATOTO KATIKA PASI YA MZAZI

Kwa utaratibu wa pasi mpya, watoto wadogo au walio chini ya umri wa miaka 18 hawataingizwa katika pasi za wazazi. Kila mtoto itabidi aombewe pasi yake mwenyewe.

F. HATI YA DHARURA [ Fomu za Hati Ya Dharura ]

  1. Hii pasi itatolewa kwa misingi ya dharura tu, na taratibu za kuomba zitafuata masharti yale yale ya pasi ya Tanzania.
  2. Mtu aliye na pasi isiyokwisha muda hatopewa hati ya dharura. Labda kwa maelezo maalumu yatakayomridhisha afisa wa pasi.
  3. Ukipoteza pasi na unataka ya dharura, itakubidi kufuata masharti yaleyale ya kupoteza pasi kama ilivyoelezwa hapo awali.
  4. Pasi hii hupatikana kwa malipo ya paundi 20.00 na katika kipindi cha ndani ya wiki moja inakuwa tayari.
    1. ulete picha 3 rangi yoyote
    2. Utajaza fomu na hainunuliwi, utaipata katika website yetu
    3. Lete kivuli cha Pasi yako
    4. Waweza kutuma maombi kwa posta lakini mahitaji yake yakamilike.

 

 

 

News and Events Visa Guestbook Trade Tourism Investment Registration

© Copyright 2003-2007 Tanzania High Commission